Thursday, January 17, 2013

"NIMECHOKA KUSEMWA...ANAYETAKA KUJUA JINSIA YANGU AVUE TWENDE KITANDANI"...ZAHARA CHAMBO WA BONGO MOVIE


MUONEKANO wa mwigizaji wa filamu za Kibongo anayefamika kwa jina la Zahara Chambo, umezua utata baada ya watu kudai kuwa ana jinsia ya kiume huku wengine wakidai ni mwanamke.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwigizaji huyo amewahi kuwa na uhusiano na mastaa kibao wa kike Bongo, lakini wote wamekuwa wazito kutoa majibu sahihi juu ya jinsia ya msanii huyo.


“Mastaa wengi tu wa kike wamekiri kuwa ‘wameshatoka’ naye lakini hawafunguki juu ya jinsia yake na namna ambavyo amewaridhisha kimapenzi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:


“Wapo wengine wanadai eti ni mwanamke na huwa anawafanyia wenzake mchezo mchafu.”


Baada ya kuyasikia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Zahara kwa njia ya simu ambapo alikiri kuwa na uhusiano na wanawake mbalimbali huku akidai huwa wanamfuata wenyewe.


“Huwa wanajilengesha kwangu kwa makusudi ili wajue kama nina jinsia ya kiume au ya kike lakini ukweli naujua mwenyewe, kama mtu anataka twende kitandani,” alisema Zahara.


Aidha aliongeza kuwa, kuna wakati wanawake wanaogopa kufanya naye kazi kwa kumhofia kuwa anaweza kufanya nao mapenzi kitu ambacho anasema hakina ukweli kwani na yeye ana mpenzi wake ambaye anampenda sana.


“Kwa hivi sasa mimi nina mtu wangu mmoja (hakutaja jinsia yake) ambaye ananipenda kuliko chochote, nashangaa kuona watu wengine wanaogopa kufanya kazi na mimi bila sababu za msingi,” alisema Zahara.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!