Monday, January 21, 2013

LADY GAGA APATA SHAVU LA KUPIGA SHOW KWENYE TAMASHA LA RAIS BARACK ABAMA -KESHO

Tamasha la Barack Obama lililokuwa limepangwa kufanyika january 19 lilisogezwa mbele hadi january 22 na badala yake likafanyika tamasha la family friends wa familia ya Obama.

The pop star Lady gaga amepata shavu la kupiga show kwenye tamasha la january 22 ambalo litakua linamhusu Barack Obama na timu yake ya kampeni ikiwa ni kumuintroduce tena Ikulu.


The Mother Monster amefuata nyayo za Jay-Z ambae alifanya tamasha kama hili mwaka 2009 baada ya ushindi wa Obama kwa awamu ile ya kwanza, ambapo Roc Nation president Jigga alibadilisha wimbo wake wa 99 Problems hasa kwenye chorus na ikasikika akimalizia kuwa but Geoge Bush Aint One. Wimbo aliubadilisha hata kipindi cha kampeni za kumsapoti Obama mwaka jana na aliibadili chorus hii na kusema but Romney Aint One.

Gaga alikua anamsapoti sana Obama katika concert kibao alizokua anapiga licha ya kuwa kuna wakati baadhi ya watu walisusia concert na kuondoka baada ya yeye kuanza kumpigia debe Obama.

Atafanya nini katika tamasha la kesho, The Mother Monster anajulikana kwa surprise kibao akiwa stage na ya kesho haijulikani itakuaje mbele ya Barack Obama.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!