Thursday, January 17, 2013

MAANDAMANO YA IFM: NILICHOJIFUNZA NI KWAMBA POLISI NI MAADUI ZETU NA SI WATETEZI
Ni vigumu sana kwa kipindi hiki kuelewa kama Askari wa Tanzania na wananchi ni maadui au ndugu.

Picha hapo juu inaonesha mmoja kati ya wanafunzi wa IFM akipokea kipigo kikali toka kwa askari wa kutuliza ghasia. 

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni pale wanafunzi hao walipoamua kuandamana kupinga kitendo cha polisi kutofanyia kazi vitendo vya uhalifu dhidi ya wanafunzi wa Hostel za Kigamboni hadi kupelekea wanafunzi hao kulawitiwa na kubakwa na wahalifu.

Askari hao walionekana kuchukua hatua ya haraka sana ya kwenda kuwatuliza wanafunzi hao pale walipoamua kuandamana. Hao hao askari walishapewa taarifa juu ya uhalifu unaoendelea Kigamboni lakini hawakufuatilia. Askari wetu wa Tanzania wanaonekana ni hodari sana kataka kutuliza maandamano ya wananchi kuliko kufuatilia uhalifu.

Maandamano yanapotokea, askari huwa wanafika eneo la tukio haraka sana na wakiwa wamekamilika kila idara. Ila wakipewa tarifa kuwa kuna uhalifu unaendelea eneo fulani, huwachukua muda mrefu hadi kuanza kufuatilia uhalifu huo. 

Kwa kifupi hakuna uhusiano/ushirikiano mzuri kati ya wananchi na askari. Kwa sasa tunaishi kama maadui. Askari wa kitanzania anahisi kupiga mwananchi ni haki yake ya msingi.

Waige mfano wa askari wa nchi za nje waone wanafanya kazi vipi. Uhusiano/ushirikiano mzuri kati ya askari wa kitanzania na wananchi unahitajika sana. Na hili linawezekana endapo askari watakua wanajitoa kuwasaidia wanachi pale wanapotoa taarifa za uhalifu, hawatakiwi kuchukulia taarifa hizo kirahisi.

TULONGE
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!