Saturday, January 12, 2013

MASTAA WANNE WALIOPIGWA "STOP" KUKANYAGA KATIKA ARDHI YA JIJI LA ARUSHA
Jambo hili linapokuwa linazungumzwa mtaani  hasa Jijini Dar utadhani ni masihara lakini lina ukweli ndani yake.Mwandishi wetu ambae alikuwa Jijini Arusha hivi karibuni alijionea madai hayo na kupata kisa kizima cha wanamuziki hao kutotakiwa kukanyaga Jijini Arusha.

Macharii hao wa Arusha ambao wanasifika kwa ukorofi walimsimulia mwandishi wetu na kumuorozeshea majina ya wanamuziki ambao wakijaribu kutia pua zao kwenye ardhi ya Jiji hilo wameisha.

KALAPINA:Kiongozi wa kundi la Kikosi cha Mizinga chenye maskani yake mitaa ya block 41 Jijini Dar.
Huyu amekuwa kwenye tageti ya masela hao kitambo kufuatia bifu lake na wanamuziki wa Nako 2 Nako ambapo miaka kadhaa ilioyopita mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo lenye umaarufu mkubwa Arusha alidaiwa kutekwa na kupigwa hadi kuvunjwa taya na wanamuziki wa Kikosi cha Mizinga hali iliyoleta uhasama hadi leo licha ya tukio hilo kutokuwa na ushahidi wa kutosha.

DIAMOND THE PLATINUM:Macharii hao walisema kuwa licha ya kosa lake sio kubwa sana lakini wanammaindi kutokana na mwaka jana kushindwa kufika kwenye onesho la muziki ambalo ilibidi atoe burudani.
Watu wengi walitoa kiingilio chao tena shilingi elfu kumi kumi matokeo yake hakufika ukumbini kwa madai ambayo baadae aliyatoa kwenye vyombo vya habari kuwa ndege ilimuacha. 
Waliongeza labda akitaka usalam aende akawaimbie shoo bure tena uwanjani na kuwaomba radhi watakuwa wameyamaliza.....

BOB JUNIOR: Utozi ulimponza,Macharii hao walisema kuwa mwaka jana mwanamuziki huyo alienda kufanya shoo lakini macharii hao waliamua kumbadilikia kwa kumrushia makopo ya maji stejini pamoja na mayai hali iliyopelekea kuokolewa na mabaunsa pamoja na polisi,kisha wakamwambia asirudi tena Jijini humo.......


OMMY DIMPOZ:Yeye amejipalia mkaa kwenye sakata lake na Load Eyez  la kumtuhumu kuiba vifaa vya gari ya Ommy hali ililosabasha mwanamuziki huyo nyota wa kundi la Nako 2 Nako kwenda jela miezi kadhaa.
.
Hali hiyo ilionekana kuwa kera sana macharii hao na kusema wanamsubiri kwa hamu kubwa aende A Town wakamletee noma.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!