Sunday, January 6, 2013

NAJMA ADAI KUWA HAJAWAHI GAWA PENZI KWA DIAMOND


BAADA ya kudaiwa kuwa msanii Najma ana mahusiano ya kimapenzi na Diamond, sasa mwenywe ameamua kuweka wazi kuwa anamfahamu Diamond kama msanii na mara nyingi wanakutana studio tu na hana muda wa kuzungumza naye ishu nyingine kama watu wanavyozusha.

Najma alifanya mazungumzo ya dakika kadhaa na mwandishi wetu maeneo ya Coco Beach, ndipo alipoweka usawa juu ya ishu hiyo, ambapo alisema kuwa hata ishu iliyokuwa inadaiwa kuwa anataka kumvisha pete ni uzushi.

“Suala la mimi na Diamond kuonana studio na kufanya kazi basi limekuwa ishu mtaani, jamani sina mahusiano na msanii huyo na wala simjui kwa chochote zaidi ya msanii tu,” alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!