Wednesday, January 2, 2013

PRODUCER LUCCI AKERWA NA DHARAU ZA WATANGAZAJI WA BONGO


Kupitia Twitter producer wa Tanzania aliyewahi kutengeneza beats za hits kadhaa ukiwemo Problem wa Cpwaa, Lucci amesimulia kiasi cha mtangazaji wa radio aliyejifanya kumsahau jina wakati wanafahamiana na alishamfanyia interview. Hata hivyo hajamtaja ni nani wala kitu cha radio anachofanyia kazi.


Lucci ameandika:
Aiseee jana kuna jambo limenikuta sasa sijui kama ilikua huyu radio presenter alikua HIGH KINYAMA au ni DHARAU KUPITILIZA…mtanisaidia.

Nilikua naingia supermarket jamaa akanipigia honi kama nikageuka akanipungia. I waved back. Wakati nnatoka nikamkuta nje tukaongea kidogo.

Baada ya story kadhaa na ma “long time man..upo?”..akaniomba number ili aje studio coz naye anaishi mbezi..nikampa number na kuanza kusepa.

Presenter huyu ambaye ashaa wahi kunifanyia interviews, na bata tukala wote na biti kuniomba,akatia “man..plz kama nikumbushe jina lako ivi”

Ilikua ni dharaaauuuuuu, ni kweli jina kanisahauuuuuuu, au dude was just ridiculously high on another level?!?!?
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!