Tuesday, January 15, 2013

PROFESA JAY AZUSHIWA KIFO....Kuna habari za uzushi zimesambaa leo kuwa rapper Joseph Haule aka Profesa Jay amefariki dunia ambazo kwa mujibu wake mwenyewe Profesa zimemshtua mama yake kwa kiasi kikubwa.


Taarifa hizo za uzushi zimedai kuwa Profesa Jay alianguka na kuzimia na wengine kudai amefariki.

Kupitia mtandao wa Twitter, Profesa Jay amezikanusha taarifa hizo kwa kuandika, “Jamani eeeh mimi ni mzima wa afya njema hao wanaozusha kuwa nimekufa wataanza wenyewe. Mi niko fresh mpaka natamani kujiteka.”

“Watu hawana kazi za kufanya kila siku kuwaombea wenzao mabaya tu maisha sijui yamewashinda wamekalia uzushi tu. Leo zamu yangu nimepigiwa simu mpaka nimeshangaa kumbe watu wanataka kuhakikisha mzee washindwe na walegee,” aliongeza.

“Imemshtua sana mama yangu maana alinisikia nilipokuwa nikioongea na moja ya simu zilizokuwa zinanipa ripoti hii.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!