Wednesday, January 9, 2013

"NAWACHUKIA SANA WASANII WA KIUME WANAOJICHUBUA"...MZEE MAGALI


MSANII nguli wa filamu za Kibongo, Charles Magali ‘mzee Magali’ amesema kuwa anachukizwa na tabia ya baadhi ya  wasanii wa kiume wa filamu wanaojichubua na kuweka dawa nywele zao.

Akizungumza na na mwandishi wa habari hii, mzee Magali alisema kwa muda mrefu amekuwa akilikemea jambo hilo bila ya mafanikio.


“Wasanii ni kioo cha jamii, hebu waseme wanapata faida gani wanapofanya hivyo zaidi ya kuhisiwa tofauti na jamii? Mbona wanaweza kuwa wasanii wazuri bila ya  kujichubua na kuweka dawa nywele zao?” alihoji.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!