Wednesday, January 2, 2013

"SITAMALIZA SIKU 7 NITAKUWA NIMEAGA DUNIA"....HAYA YALIKUWA NI MANENO YA MWISHO YA SAJUKI KWA ROMAKupitia ukurasa wake wa Facebook rapper wa 2030, Roma Mkatoliki amesimulia maneno ya mwisho aliyoambiwa na marehemu Sajuki.


NINACHOKUMBUKA SHOW YA MWISHO ARUSHA YA KUMCHANGIA SAJUKI!!TUKIWA CHUMBANI KWAKE MIMI, WASTARA, DJ CHOKA, YUSUPH MLELA NA WENGINEO, SAJUKI ALIMSHIKA MLELA MKONO HUKU AKIMTAZAMA KWA HUDHUNI NA AKAMWABIA:

“SITAMALIZA SIKU 7 NITAKUWA NIMEIAGA DUNIA” 


ILIKUWA HARD TYM SANA KWETU NA WENGI TULILENGWA NA MACHOZI KWA KAULI ILE!!

LEO LIMETIMIA LILE NENO…oooh god mfutie dhambi zake na muepushe na adhabu za huko!! nasisi tupate somo kuwa maisha yanaweza yakabadilika within a second!!Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie na apumzike kwa amani!!! poleni sana marafiki wenzangu.

Msiba wa sajuki upo nyumbani kwake maeneo ya tabata bima, na marehemu sajuki anategemewa kuzikwa siku ya ijumaa hii .yote ni kuwasubiri ndugu kutoka mkoani Ruvuma..
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!