Monday, January 14, 2013

TENGA AUKIMBIA "URAIS" WA TFFRais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amesema hawezi kugombea tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo unaotarajia kufanyika February 24 mwaka huu.


Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Tenga amesema wakati anaingia madarakani miaka minne iliyopita alikuwa na kazi ya kufanya, ambayo ilikuwa ni kujenga taasisi ya soka nchini, na kwamba hawezi kuendelea tena kwani uongozi ni kijiti na kwamba huu sasa wakati wa kukimbizwa na mtu mwingine.

“Nimekaa madarakani kwa miaka minane kwakweli ni miaka mingi sana,tangu mwaka 2004 ambapo wakati huu kulikuwa na ajenda maalum ya kuleta mabadiliko ya msingi katika soka”alisema Tenga.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!