Saturday, January 19, 2013

VIDEO YA KIM KARDASHIAN ALIPOITIKISA IVORYCOAST....


Mwaka huu mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan umekuwa na bahati ya kutembelewa na mastaa wa Marekani ambapo mwanzoni kabisa mwa mwezi huu Chris Brown na Rihanna walikuwa huko kuhudhuria tuzo za Kora. 

Na sasa mrembo anayezungumzwa zaidi kwenye internet, Kim Kardashian ameenda kutalii kwenye mji huo. Kim alithibitisha taarifa hiyo kupitia Twitter kwa kuandika:
kim africa
Amekwenda huko kwenye hafla ya uzinduzi wa simcard ya Ma Life ya mtandao wa simu wa Orange itakayofanyika leo jioni.

Kabla ya kwenda nchini humo Kim na mpenzi wake Kanye West ambao hivi karibuni walitangaza kutarajia mtoto walikuwa wote jijini Paris.

VIDEO....
 
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!