Monday, January 21, 2013

"BABY WANGU ANADEKA SANA JAMANI.....YAANI WASIOPENDA PENZI LETU IMEKULA KWAO"...AMANDA


STAA wa filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa kipenzi chake, Emmannuel Rushau ‘Bwana Misosi’ anapenda kudeka pindi wanapokuwa viwanja.


Akiongea  kwa mbwembwe namwandishi wetu katika Viwanja vya Leaders Club hivi karibuni, Amanda aliweka wazi kuwa mpenzi wake huyo amekuwa na tabia hiyo hali ambayo inaleta maswali mengi kwa wasiolipenda penzi lao.


“Jamani Baby wangu naye anadeka... hebu tazama sasa hivi alivyonilalia, majungu yataanza sasa hivi. Lakini nilikuwa nikiomba faraja, sasa nimeipata nashukuru,” alisema Amanda.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!