Thursday, January 17, 2013

WEMA SEPETU AMALIZA BIFU NA MAMA YAKE....


MWANADADA sura ya mauzo katika filamu za Bongo, Wema Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu wamemaliza bifu lao, sasa ukiwaona ni kama kumbikumbi......

Hivi karibuni kwenye Arobaini ya mama wa Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema, nyumbani kwao Kinondoni-Studio, Dar, Wema alibambwa akimfuata mama yake aliyekuwa pembeni na kumkumbatia huku akimdekea.


Mama na mwana hao waliendelea kubembelezana na kuwafanya watu waliokuwa eneo hilo kuwashangaa kutokana na kumbukumbu za hivi karibuni ambapo walitofautiana kiasi cha Wema kukataa mama yake asifike kwake.


Akizungumza na  mwandishi wetu baada ya kuwakuta wamekumbatiana, mama Wema alisema:


“Nampenda sana mziwanda wangu huyu, we’ acha tu, japokuwa muda mwingine ananikosea. Unajua napenda kuwa naye muda wote lakini kutokana na majukumu aliyonayo kuonana ni tabu, lakini Wema kwangu bado ataendelea kuwa mtoto siku zote.” 


Aidha, wakiwa wanaendelea kupiga stori za hapa na pale, mama huyo alimchombeza bintiye kuhusu kula ice cream

ambapo Wema alidakia na kumwambia mama yake kuwa asijali wakimaliza shughuli za arobaini hiyo watakwenda.

“Usijali mama yangu, tukimaliza hapa tutakwenda. Mimi nipo wala huwezi kukosa kitu ambacho unakitaka,”
alisema Wema. 


Mwishoni mwa mwaka jana, Wema alimkasirikia mama yake huyo kufuatia kuanika runingani mambo ambayo binti yake hakuyapenda yawe wazi.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!