Thursday, January 17, 2013

"MAPENZI YAMENIPOTEZEA MUDA NA KUNIFANYA NUJUTE"....NISHA


STAA wa la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa anajuta kupoteza muda mwingi kwenye mapenzi kuliko kazi mwaka jana.

Akiongea na mwandishi wetu, Nisha alisema amebaini kuwa mwaka 2012 mapenzi yalimfanya ashindwe kutimiza malengo yake mengi kwenye soko la filamu.


“Mwaka jana nilipelekwa puta sana na mapenzi. Mara kigogo, Geofrey na Nay wa Mitego jambo ambalo lilinifanya nishindwe kufanya kazi kwa ufanisi. Mwaka huu sikubali, mwendo wa kazi tu siyo mapenzi,” alisema Nisha.


Aidha, aliongeza kuwa atahakikisha anashirikiana vizuri na wenzake katika kazi zake.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!