Friday, February 1, 2013

NIMEMALIZA KWA LULU NAHAMIA KWA KAJALA"..DK. CHENI


STAA aliyekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ anapata dhamana, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amefunguka kuwa baada ya kufanikiwa kwa Lulu sasa anahamia kwa msanii mwingine, Kajala Masanja.     

Akizungumza nje ya Mahakama Kuu jijini Dar baada ya Lulu kuachiwa, Dk. Cheni alisema kwa sasa anaanza mchakato wa kumsaidia Kajala mpaka ajue hatima ya kesi  inayomkabili.

“Unajua Lulu siyo mtu wa kwanza kumsaidia na mama yake ndiye aliniomba, nilishawasaidia wengi. 


Hata Cloud alipofungwa nilifuatilia mimi na Dude mpaka mwisho, hatukukata tamaa na kwa Kajala nitafanya hivyo kwa sababu ni mwenzetu jamani, naamini Mungu anaweza sana na atafanikisha kila kitu,” alisema Dk. Cheni.

Kajala anasota Segerea akikabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa bondi na serikali kutokana na mumewe kutakatisha fedha haramu.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!