Monday, April 11, 2016

Anne Kilango Malecela: Sijapata taarifa ya 'Utenguzi' kutoka kwa aliyeniteua.


Leo taarifa ambayo metrend vya kutosha kwa muda mfupi, ni kuhusu Rais wa J.M wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi hiyo.

Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa.

Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi unaendelea.

Sasa Mtangazaji wa Sun Rise, Stanslaus Lambert, amezungumza kwa simu na Mbunge huyu wa zamani wa Same Mashariki ambapo amedai yeye hana taarifa ya utenguzi wake kutoka kwa Rais.

“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.

Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!