Saturday, April 2, 2016

Siku tatu za mwanzo baada ya ‘Ndindindi’ zilimtesa Lady Jaydee

Lady Jaydee amefunguka kuwa siku tatu za mwanzo baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Ndindindi’ zilimpa shida na hakutegemea wimbo ungepokelewa kama ilivyo sasa.

Lady Jaydee aka Commando, Anakonda na majina mengi aliyopewa kutokana na ujasiri wake na uwezo wa kujituma ni miongoni wa wasanii wachache wa Bongo waliokaa kimya kwa kipindi kirefu lakini wakarudi kwa kishindo.

Akizungumza kwenye kipindi cha The Chart Show, kinachoruka kupitia Times FM, Lady Jaydee amesema, ‘Nilijua kuwa wimbo utafanya vizuri lakini baada ya kuachia wimbo siku tatu za mwanzo nilipata shida’.

“Nilijua kuwa wimbo wa ‘Ndindindi’ utafanya vizuri, lakini sikutegemea kama utapokelewa kama hivi ilivyokuwa sasa. Tangu naanza zile siku thelathini nilijua nitafanya vizuri lakini baada ya kuachia wimbo siku tatu za mwanzo nilipata shida sana, nilikuwa ni kama mtu aliye graduate shule unafikiria atakuwa kwenye hali gani,” aliongeza Jaydee.

Ndindindi umebahatika kupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki na pia unafanya vizuri kwenye vituo vya redio mbalimbali.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!