Monday, May 23, 2016

Ajali ya Lori Kuua Watu Nane Chunya.


Watu wanane wafariki dunia na wengine wajeruhiwa mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka katika Mlima Sayini Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Lori lililokuwa limebeba mitumba ya wafanyabiashara lilitoka katika kijiji cha Upendo, baada ya mto Luba mpakani mwa halmashauri ya mji mdogo wa Makongolosi na Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Chunya Dr.Ano Maseta,alisema kuwa watu wanane waliofariki kati yao wanaume saba na mwanamke mmoja.Watu waliofikishwa hospitalini hapo ni 62,kati ya hao wanane walikuwa wameshakufa,lakini majeruhi 54 wametibiwa hospitalini hapo

"Kati yao Majeruhi saba walipelekwa hospitali ya rufaa mkoa wa Mbeya kutokana na hali zao kutokuwa nzuri",alisema Dr.Ano.

Wakizungumza na Mwandshi wetu ndani ya Hospitali hiyo, baadhi ya majeruhi walisema kuwa gari hilo lilikuwa limejaa abiria na walipofika kwenye mlima Sayini lilikuwapo gari kubwa la lveco mali ya kampuni ya Uchimbaji Madini la Sun Shine lilikuwa likitokea mbele na lilikuwa limewasha taa zenye mwanga mkali.

Mmoja wa majeruhi hao alisema kuwa kutokana na mwanga huo dereva alishindwa kumudu gari ukizingatia ilikuwa mwendo kasi."Dereva wetu alishindwa kumudu gari kutokana na mwanga wa gari lililokuwa linakuja mbele yetu pia alikuwa akiendesha kwa kasi.Hivyo nlishtukia gari limeanguka na watu walikuwa wakilia kwa sauti",alisema.

Mwenyekiti wa wilaya ya Chunya,Bosco Mwanginde alifika katika eneo la tukio na kushuriki kuwabeba majeruhi hao.Mwanginde aliwataka wafanyabiashara wa mitumba kuacha  kutumia malori wanapokwenda katika biashara zao.Pia alisema kuwa ni wakati sasa kikosi cha usalama barabarani kufuata taratibu na kanuni za nchi na kuchukua hatua kwa wale wote wanaobeba watu katika malori.

Mwanginde alisema kuwa hii ni ajali ya pili kutokea kwani ajali nyingine ilitokea jumatano ambapo lori lililokuwa limebeba wafanyabiashara wa mitumba na kuua watu 24. 

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!