Sunday, May 22, 2016

Godbless Lema ataka kufungwa kwa vifaa bungeni vinavyopima ulevi. Ampongeza Rais Magufuli kwa kumfuta kazi Waziri Kitwanga.


Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani amabye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Godbles Lema ameshauri kufungwa kwa vifaa maalum vinavyopima ulevi ndani ya bunge ilikulinda heshima ya Mhimili huo wa Bunge.

Waziri huyo kivuli pamoja na mambo mengine amepongeza uamuzi wa Rais wa kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nje Charles Kitwanga huku akisema ni dhahiri kiongozi huyo amechafua hadhi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Lema amekiri kitendo cha unywaji wa Pombe kupitiliza kwa kiongozi ni utovu wa nidhamu jambo ambalo huenda likazidi kushusha hadhi ya bunge ambalo ni Mahususi kwa kutunga sheria na kuisimamia Serikali.

Haya yanakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya taarifa ya Ikulu ya Dar es Salaam kutangaza kumtimua kazi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi baada ya kuingia bungeni na kujibu swali la wizara yake kimakosa huku akiwa amelewa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!