Monday, May 30, 2016

Hali Tete Zanzibar
Hali ya siasa kisiwani Zanzibar inazidi kuwa tete,baada yaq jana polisi kurusha risasi na kutupa mabomu ya machozi kuwasambaratisha wafuasi wa Chama cha Wananchi  CUF Maalim Seif Hamad.
 Maalim juzi
alianza ziara yake ya siku sita katika visiwa vya Unguja akitembelea ofisi za chama hicho na kifanya vikao vya ndani.Polisi walilazimika kufyatua risasi juu na kutupa mabomu ya machozi katika eneo la Bumbwini katika ofisi za CUF na kuwatawanya wafuasi na wapenzi wa chama hicho.

Wafuasi hao walikuwa wamejipanga kando ya barabara kumlaki kiongozi wao.Kutokana na vurumai hiyo polisi walilazimika kuzuia msafara wa Maalim Seif,kwa saa moja akiwa njiani kuelekea kijiji cha Bumbwini.

Maalim alikuwa na kikao cha ndani cha kichama katika ziara zake za kawaida wilaya ya kaskazini B unguja.Msafara wa Maalim ulipofika katika barabara za michungwa miwili njia ya kuelekea Bumbwini,polisi waliwazuia na kuwaamuru wawatawanye wafuasi wao waliokusanyika kijijini hapo.

Polisi walilizunguka gari la Maalim Seif wakiwa na silaha za kila aina na kumtaka kiongozi huyo awatume wajumbe wachache wakawatawanye wafuasi wao.Polisi pia waliruhu magari machache na watu wachache ndiyo waendelee na msafara  huo huku wakiagiza baadhi ya watu waziende kwenye vikao hivyo.

Agizo jingine waliolitoa ni watu waliokuwa nje ya jengo ambapo kikao kilikuwa kinafanyika waliwaamuru waondoke ili kuimarisha ulinzi.Polisi pia walizuia matumizi ya vipaza sauti ingawa walifunga kamera za ulinzi zilizokuwa zikirekodi matukio yote.

Maalim Seif akiongea katika kikao hicho alisema kuwa mabomu na risasi wanatumia dhidi ya waqfuasi wa CUF zinatishia ukuaji wa uchumi unaotegemea watalii.Pia alisema kuwa kitendo hicho ni kuvuruga amani ya nchi.

"Polisi jizuieni mnafanya kazi ya nani na mnawalinda wananchi au Chama cha Mapinduzi....sisi mkitupiga masbomu ndo tunanawiri vizuri katika ulimwengu wa siasa na nyie mnazidi kupoteza chama chenu.Sisi tunaweza kuonesha dunia kuwa tunaweza kuongoza bila kumwaga damu."alisema Maalim Seif.

Alisema kuwa kila wanachofanyiwa na polisi ni ushahidi wa kuupeleka katika mahakama ya kimataifa inayohusika na makosa ya jinai(ICC).Pia alisema Wazanzibar wanataka mabadiliko pamoja na kuwa wamefanyiwa mbinu za kuzuiwa lakini wao hawakuyumba kufanya jambo ambalo ni haki yao kufanya mikutano ya kichama.

Aliasema CUF bado wanaendelea na msimamo wa kutomtambua Rais wa Zanzibar,Dr.Shein na serikali yake.Pia alisema kuwa tangu novemba mwakajana Zanzibar haina serikali halali wala rais halali kwa kuwa aliyepo ameingia kwa hila.

"Tulifanya uchaguzi na waangalizi wa ndani na nje walithibitisha kuwa uchaguzi ulikuwa wa huru na haki lakini Jecha alifuta uchaguzi wa Zanzibar tu wakati Tanzania nzima uchaguzi ulikuwa siku mija tu."
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!