Sunday, May 22, 2016

Mashindano ya Big Brother Africa yaahirishwa Tena kwa Mara ya Pili

 Kama ulikuwa unasubiria kuona mashindano ya Big Brother Africa basi pole sana sababu kwa mwaka huu hayatakuwepo.
Mashindano ya Big Brother yametokea kuwavutia watu wengi kutokana na kukutanisha washiriki wanaotoka mataifa mbalimbali ya Africa, huku Tanzania ikionekana kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo kupitia M-Net wamesema kwa sasa wanajiandaa kuweka mikakati ili kuboresha mashindano hayo hapo mwakani.
 
 Mpaka sasa taji hilo la Big Brother linashikiliwa na Idris Sultani aliyefanikiwa kushinda mwaka jana na kupata zawadi ya fedha kiasi cha dola laki tatu
 
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!