Monday, May 23, 2016

Mbunge Alalamika Kuhusu Sheria ya Mtandao.

WIZARA ya Uchukuzi na  Mawalisiliano,imetakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya sheria ya mtandao iliyopitishwa mwakajana.

Mbunge wa viti Maalum Oliver Semunguruka (CCM),alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akichangia mjadala wa bajeti ya wizara hiyo bungeni mjini Dodoma.

Semuguruka alisema kuwa  sheria hii bado haijafahamika vizuri kwa wananchi kwa kuwa imekuwa ikitafsriwa vibaya na watu kwa sababu hawaelewi vizuri.

Elimu juu ya sheria ya mtandao bado haijawafikia wananchi wengi na wadau wengi hapa nchini.Hivyo Wizara husika ihakikishe inawapa elimu ya kutosha ili itumike ipasavyo.

"Pamoja na hayo, lazima pia serikali ihakikishe kampuni za simu zinatumia gharama sawa katika matumizi ili kuwasaidia wananchi kupunguza gharama katika simu.

"Nasema hivyo kwa sababu mkongo wa taifa umeenea nchi nzima,lakini bdo kuna maeneo yanashida katika huduma za mtandao wa mawasiliano wakati kuna baadhi ya kampuni zikipokea ruzuku za kupanua huduma hizo vijijini.Ukosefu wa huduma za simu vijijini inasababisha usumbufu kwa wananchi kubeba zaidi ya simu tatu zenye mitandao tofauti kwa wakati mmoja.Hivyo ni vyema Serikali iboreshe huduma hiyo ili kuondoa usumbufu huyo".alisema semuguruka.

Pamoja na hayo Mbunge huyo alizitaka kampuni za simu nchini kuanza kuuza hisa zao katika soko la hisa ili kufanya wananchi waweze kumiliki sehemu ya hisa hizo na kufanya mapato  na matumizi yao kuwa wazi.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!