Saturday, May 21, 2016

POLISI YASHIKILIA WATU 8 KWA UJAMBAZI

                                Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es saalam
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wanane wakihusishwa na tukio la ujambazi wa kutumia silaha baada ya mwenzao mmoja kukutwa na bastola iliyokuwa na risasi tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema Mei 13 mwaka huu saa 2:00 usiku katika eneo la Mbezi Beach njia panda ya Goba, walifanikiwa kukamata bastola aina ya Browning namba 6.35 ambayo alikuwa nayo mtuhumiwa Waziri Jamali (39) mkazi wa Mbezi.

“Silaha hiyo ilipatikana baada ya askari kupata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna kundi la watu wanaojihusisha na ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo hayo, askari walifika na kumkamata mtuhumiwa huyo,” alisema.

Mtuhumiwa huyo katika mahojiano alikiri kuhusika katika matukio kadhaa ya ujambazi na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea wa tukio hilo ili kubaini uhalali wa silaha hiyo na kujua matukio waliyowahi kufanya na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Kamanda Sirro alisema polisi pia inamshikilia Wenceslaus Mtui (46) mkazi wa Makongo Juu kwa kosa la uuzaji wa madini bandia.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!