Monday, May 23, 2016

Sekondari ya Al Muntazir yakiuka Agizo la Serikali.


Uongozi wa shule ya Muntazir Dar es salaam imeendelea kukiuka agizo la serikali la kutopandisha Ada hadi pale Serikali itakapotangaza ada elekezi. 

Shule hiyo inadaiwa kupandisha ada kwa kwa asilimia 10  kutoka ada ya awali waliokuwa wanalipa wazazi hao.

Baadhi ya wazazi waliueleza  mtandao huu kuwa awali wanafunzi wa shule ya msingi walikuwa wanalipa Sh.128,0000 lakini hivi sasa ada imepanda na kufikia Sh.248,0000 kwa mtoto mmoja ambapo ni ongezeko la Sh.660,000 kwa mwaka

Chanzo hicho kilidai kuwa wanafunzi wanaosoma shule ya awali wanalipa Sh.158,0000 kwa sasa wanatakiwa kulipa Sh.1980,000 huku wazazi wanaochelewesha kulipa ada wakikabiliwa na adhabu ya sh, 100000

Akizungumza mmoja wa wazazi hao alisema kuwa,anashangaa shule hiyo kupandisha ada bila kuogopa tamko la serikali la kutopandisha ada hadi ada elekezi itakapotolewa.

"Mbali na tamko hilo pia zipo shule 45 ambazo ziliomba Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknologia na Mafunzo ya Ufundi kupandisha ada lakini Al MUNTAZIR si miongoni mwake ingawa hakuna hata shule moja iliyokubaliwa kupandisha ada"alisema Noor Mohamed.

Noor mohamed alisema kuwa shule hiyo iliandika barua kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam na kamishna wa mkuu wa mkoa aliuandikia barua uongozi wa shule hiyo mach 25 akiupa siku saba kurejesha ada ya zamani lakini uligoma kufanya hivyo.
 
Alisema kuwa wazazi walipeleka malalamiko yao kwa Waziri mwenye dhamana,Pro,Joyce Ndalichako ili wapate ufafanuzi juu ya ongezeko hilo.Naibu Mkurugenzi wa  Utaratibu na uendeshaji wa shule hiyo,Muddasir Masi alisema shule imeongeza ada kutokana na ubora wa elimu inayotolewa shuleni hapo.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!