Monday, May 30, 2016

Serikali Kuingilia MauajiSiku chache baada ya familiya ya Erasto msuya,aliyeuwawa kwa kupigwa risasi 12 mwaka 2013,kuiomba serikali kuwapa ulinzi huenda kilio chao kikasikilizwa.
Kilio hicho kinaweza kupatiwa ufumbuzi baada ya kuwapo kwa taarifa ya viongozi kuwa leo watashiriki kwenye ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Anethe Msuya ambaye ni mdogo wa marehemu Erasto.

Anethe aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake eneo la Kibada jijini Dar es salaam.Juzi familia ya Bilionea Erasto Msuya,ilimuomba Rais John Magufuli luingilia kati mauaji yanayoendelea katika familia yao kwa kuwawekea ulinzi wa jeshi la polisi huku wakitaka Mahakama zinazoendesha kesi hizo kufanya uchunguzi wa kina.

Waziri Mkuu,Khasim Majaliwa na Waziri wa Fedha na Mipango,Dk.Philip Mpango wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Anethe aliyekuwa akifanya kazi kwenye wizara ya fedha na mipango.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa saa mbili asubuhi kibada na  saa nne utapelekwa nyumbani kwqa dada yake Mbezi Salasala.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo majira ya saa tisa atasaliwa katika kanisa la KKKT Salasala,na baadae safari ya kuelekea Arusha kwa mazishi itaanza.

Marehemu Anethe Erasto ni mdogo wa Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 12 agasti 7 mwaka 2013 jirani na kiwanja cha Kilimanjaro(KIA).

Anethe umauti ulimkuta uliosababishwa na kuchinjwa kinyama yaliyotokea mei 26 mwaka huu huko nyumbani kwake kibada.Marehemu ameacha mtoto mmojaq Allan Kimario(4)ambaye pia aliweza kushuhudia wauwaji hao wakiingia katika nyumba hiyo aliyokuwa akiishi mama yake.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!