Friday, May 20, 2016

Tanzia: Askari wa Usalama Barabarani, Ally Kinyogoli Auawa kwa Kupigwa Risasi.

Watu wasiojulikana wakiwa na pikipiki aina ya Boxer,usiku wa kuamkia leo wamemuuwa kwa kumpiga risasi kadhaa katika sehemu mbalimbali za mwili wake Askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani, Ally Kinyogoli nyumbani kwake Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.

Baada ya kumuua, watu hao walitokomea kusikojulikana bila kuchukua kitu chochote

Kinyogoli alijizolea umaarufu katika kipindi cha redio One kila siku asubuhi alipokuwa akitoa taarifa za hali za barabarani zikiwemo njia zenye foleni kwa wakazi wa jijini.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!