Wednesday, May 25, 2016

UVCCM Yawavaa Wanaomkosoa Rais Magufuli


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umelaani kitendo cha baadhi ya wananchama wa vyama vya upinzani kumbeza Rais John Magufuli na kumuita dikteta kutokana na kuendelea kutumbua majibu ndani ya Serikali yake.

Naibu Katibu Mkuu wa Oganizasheni na Siasa ya UVCCM Taifa, Pilly Mbanga alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na wananchama wa CCM mjini Morogoro wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na jumuiya zake. 

Mbanga alisema UVCCM wanaunga mkono utendaji wa Rais Magufuli na hawatakubali kamwe kauli zinazotolewa na wapinzani zinazolenga kumkatisha tamaa.Alisema anafanya hivyo kwa lengo la kutetea wanyonge.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!