Monday, May 30, 2016

Waliotimuliwa UDOM Wazagaa Mitaani
Wanafunzi 7000 walioamriwa kuondoka Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) ndani ya muda usiozidi masaa 24 wameonekana wakirandaranda mitaani baada ya kukosa makazi.
Uongozi wa Chuo hicho juzi ulitoa tangazo kwa wanafunzi hao kuwa unawataka wanafunzi hao kuondoka chuoni hapo kutokana na kufutwa kwa programu hiyo maalum kutokana na tatizo la ufundishaji.

Wanafunzi hao wamelazimika kurandaranda mitaani kutokana na madai ya kukosa fedha za kurejea majumbani mwao wala kulipia vyumba vya kulipia wageni.

Aidha,hata waliokuwa na fedha za kulipia malazi,walikumbana na kikwazo cha nyumba za wageni kutokuwa na nafasi nkutokana na vikao vya bunge la bajeti,vinavyoendelea tangu Aprili 16,mwaka huu.

 Kadhia hiyo imewakumba wanafunzi wa mwaka wa kwaza na wa pili,wanaosoma programu maalum iliyoanzishwa mwaka 2014,chini ya Rais wa awamu ya nne,Jakaya Kikwete,akilenga kuondoa upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari nchini.

Tangazo lililotolewa juzi na uongozi wa Udom kwa wanafunzi hao,kufuatia uamuzi wa serikali kupitia Wizara ya Elomu,likiwataka wanafunzi hao kuhakikisha ifikapo jana,saa 12;00 jioni wawe wamekonda chuoni.

Wanafunzi hao walielezea kushangazwa na hatua iliyofikiwa na serikali kwamba hawakutarajia kutokea kitu kama hicho.Walisema wanachofahamu chuoni kulikuwa na mgomo wa walimu ambao walikuwa na madai ya malimbikizo ya malipo ya mishahara yao na si jambo jingine.

Mmoja wa wanafunzi anayesoma mwaka wa pili,kwa sharti la kutotaja jina lake amesema kuwa,kwa wiki mbili kabla ya tangazo la kuwatimua wanafunzi hao halijatangazwa,walikuwa hawafundishwi kwa sababu ya mgomo wa walimu na kwamba hatua hiyo ya serikali kuwafukuza imewatia hofu.

Ilielezwa katika tangazo hilo, kuwa uamuzi huo uilitokana na kuwepo kwa matatizo ya ufundishaji katika kozi hiyo.Alisema hofu hiyo imetokana na kutojua hatima ya masomo yao kwani kozi hiyo inapatikana Udom tu.
 
Mwanafunzi mwingine alieleza kuwa serikali haijawatendei haki kutokana na kuondoka chuoni bila kuelezwa sababu za msingi,zaidi ya kuelezwa kuwa watapelekewa taarifa za hatima ya masomo,mapema yao,mapema iwezekanavyo.

"Wengine taarifa tumezipata jana na wengine leo asubuhi,hivyo uongokaji utakuwa tofauti  lakini wengi waliokuwa na nauli wameondoka leo asubuhi,wengine hawana nauli mpaka sasa wapo pale chuoni wanasubiri ndugu zao wawatumie fedha."alisema mwanafunzi huyo.

Baadhi yqa wanafunzi wanashangazwa na magari ya polisi aina ya defender yalikuwa yakizunguka nje ya chuo hicho.Walisema bila shaka halihyo ilitokana na polisi kudhani kuwa wanafunzi wangeweza kufanya vurugu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!