Monday, June 13, 2016

Askari wa wanyamapori aliyesema bora wauawe binadamu 100 kuliko Tembo mmoja kuchukuliwa hatua.


Siku  mbili baada ya kituo cha ITV kurusha  taarifa ya wananchi wa kijiji cha Likuyumandela kusumbuliwa  na Tembo na kusababisha kifo cha mwananchi mmoja  Naibu waziri wa maliasili na utalii amefanya ziara katika  kijiji hicho huku akikiri ziara hiyo imefanyika baada ya kuona taarifa kwenye kituo cha ITV ambapo  ameagiza uchunguzi ufanyike kwa  askari wa wanyamapori aliyesema bora wauawe wananchi mia moja kuliko Tembo mmoja  ili hatua zichukuliwe   dhidi yake.

Naibu waziri huyo wa maliasili na utalii Mhandisi Ramo Makani amefanya ziara ya ghafla akiwasili  kwa  ndege katika jijiji hicho   baada ya kuona  taarifa kwenye kituo cha ITV kuhusiana na  wananchi wanavyosumbuliwa na Tembo ambapo pia ametembelea mashamba  ya wananchi yaliyoharibiwa  na Tembo na kwenda kuwapa pole  ndugu wa marehemu Yasin Antonio aliyeuawa kwa kukanyagwa na Tembo huku akilaani kauli ya kwamba heri wauawe  binadamu  mia  moja kuliko Tembo mmoja.
Mheshimiwa Ramo Makani ameagiza taratibu zifanyike kwa maeneo mbalimbali nchini kunakotakiwa wananchi kulipwa kifuta jasho na kifuta machozi taratibu zikamilishwe ili serikali ijue  kiasi cha pesa inachodaiwa huku pia akiagiza taratibu za usajili wa kijiji cha Likuyu mandela zifanyike na kuagiza kupelekwa kwa askari wanyamapori kwa ajili ya kufanya doria  katika kijiji hicho.
Awali wananchi wa kijiji cha Likuyu mandela chenye wakazi zaidi ya 3500  walieleza malalamiko yao mbele ya naibu waziri huyo wakisema licha ya wao kuwa  mstari wa mbile katika harakati za uhifadhi wa maliasili lakini viongozi wamekuwa hawachukui hatua wanapopelekewa malalamiko yao.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!