Tuesday, June 14, 2016

Balozi wa China kuchangia damu Muhimbili Leo


 Balozi wa China nchini Tanzania ameungana na watanzania katika kuchangia damu kwa hiari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mchangia damu duniani.

Akiongea wakati wa shughuli hiyo ya uchangiaji damu Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Makwiya Makani amesema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa damu kwa asilimia 25.

Dk. Makani ametoa takwimu hizo leo jijini Dar es Salaam alipomkaribisha Balozi wa China hapa nchini Dk. Lu Youging alipotembelea hospitalini hapo kwa lengo la kuchangia damu ikiwa ni katika maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mchangia damu duniani.

Dakta Makani amesema kuwa mahitaji halisi ya damu ni chupa 100 hadi 130 kwa siku, lakini chupa zinazopatikana kwa siku ni 60 hadi 100 pekee ambapo mgonjwa mmoja aliyeafanyiwa upasuaji wa moyo anahitaji kuongezewa chupa 6 za damu.

Kwa upande wake mkuu wa Idara ya Maabara kuu Dk. Alex Magesa amesema kuwa hivi sasa ambapo shule zimefungwa na waumini wa Kiislamu wakiwa katika mfungo,kasi ya kujitolea damu imepungua sana hivyo kunaweza kutokea upungufu mkubwa zaidi.


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!