Wednesday, June 15, 2016

Bodi ya mikopo nchini yapewa wiki 2 kuwachukulia hatua za kisheria watumishi waliosimamishwa kazi


Serikali imetoa wiki mbili kwa bodi ya mikopo nchni kuwafungulia mashtaka kwa mujibu wa sheria watumishi waliosimamishwa kazi kutokana na udhahifu uliobainika katika mfumo mzima wa usimamizi katika utoaji na urejeshaji ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa kusababisha wizi na ubadhirifu wa fedha za walipa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari kutokana taarifa ya uchunguzi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi. Profesa Joyce Ndalichako pia ameitaka bodi hiyo kuwa na maelezo ya kina kuhusu wanafunzi wa 168 wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wanaokopeshwa zaidi ya milioni 531.3 pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma 919 wanaoonekana kukopsehwa zaidi ya bilioni 2.530 na hakuna utambulisho wa wananfunzi hao vyuoni wala ushahidi wa fedha hizo kurejeshwa bodi ya mikopo.
Aidha amesema bodi ya mikopo nchini imetumia makampuni ya udalali kukusanya madeni kwa wanafunzi kwa makubaliano ya malipo ya Asilimia 2.5 ya deni la mdaiwa, ambayo makampuni mengine hayajasajiliwa na mengine yamesajiliwa kuuza vifaa vya ujenzi wakati wadaiwa wanawadhamini na kusababisha watu kubambikiwa madeni ili madalali wapate kamisheni kubwa.
Kuhusu baadhi ya benki kutaka kutoa taarifa za miamala ya fedha za serikali zilizopelekwa kwa wanafunzi mbalimbali, Prof Ndalichako ametoa wito kwa mabenki yote kutoa ushurikianao na kusistiza benki yoyote itakayokaidi agizo la serikali itasitishiwa kutumiwa na serikali kupitisha fedha kwa ajili ya wananfunzi hao.
Aidha amesema kwa sasa serikali imesimamisha mfumo wa kufanya ulinganifu wa sifa zinazotokana na vyuo nya nje ya nchi vilivyo na matawi hapa nchni mpaka itakapofanya utafiti wa sifa zinazostahili kutokana na baadhi ya wanafunzi wa vyuo hivyo kulalamikia gharama kubwa zinazotozwa huku vikitumia walimu wa hapa nchni.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!