Saturday, June 18, 2016

Breaking News: Jeshi la Polisi Lawatawanya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Dodoma Ambao ni Wafuasi wa Chadema Kwa Kufanya Mahafali Bila Kibali


Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma  limesambaratisha wanafunzi  wa vyuo vikuu  wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO ) waliokuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika  Ukumbi wa African Dreams  ulipo Area D mjini Dodoma.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi walikamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao. 

Polisi wamesema mikusanyiko  yote ya kisiasa ilishapigwa marufuku, hivyo hata mahafali hiyo ilikuwa batili

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!