Thursday, June 23, 2016

Dkt. Magufuli-kuziba midomo ni Demokrasia ya aina yake...cha Msingi Maendeleo Kwanza


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka wanasiasa kuachana na harakati za siasa katika kipindi hiki mpaka baada ya miaka mitano ili kutoa nafasi ya kutekeleza ahadi alizozitoa kwa ajili ya Maendeleo na Watanzania na nchi kwa ujumla.

Akizungumza leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amewataka wanasiasa waliopewa nafasi za uwakilishi na wananchi wajikite zaidi katika kuwahudumia ili kuwaletea maendeleo waliyowaahidi wakati wa kampeni.

Rais Magufuli amesema kuwa wakati wa uchaguzi umekwisha hivyo wakati wa siasa sasa nao umekwisha hivyo amewataka viongozi wao wa siasa kushirikiana nae katika kuleta maendeleo ikiwemo kumpa ushauri ambao nae ataufanyia kazi kwa maendeleo ya Wananchi wote.

Dkt. Magufuli amesema kuwa kamwe hatomvumilia mtu yoyote ambae atamchelewesha katika harakati zake za kuwaletea maendeleo wananchi, hivyo ni vyema wakaungana kwa pamoja katika kufanikisha suala hilo.

Rais Magufuli amesema wabunge waliochaguliwa waelekeze nguvu katika kuwasemea wananchi kwa kufuata demokrasia ingawa hata kuziba midomo ni demokrasia ya aina yake lakini amevitaka vyama vyote kushirikiana nae katika kulileta taifa maendeleo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!