Monday, June 27, 2016

Dogo Janja awatiamoyo mashabiki wa Diamond baada ya kukosa tuzo ya BET


Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amewataka mashabiki katika mitandao ya kijamii kuacha kuandika maneno ya kumbeza Diamond Platnumz baada ya kukosa tuzo ya BET na kuchukuliwa na Black Coffee kutoka Afrika Kusini.

Rapper huyo ambaye ameachia remix ya wimbo ‘My Life’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha Radio & Weasel kutoka Uganda, ameiambia Bongo5 kuwa hatua aliyoifikia Diamond kimataifa ni kubwa hivyo anapaswa kupongezwa.

“Unajua watu walikuwa wanamatarajio makubwa sana na tuzo lakini mwisho wa siku tukubali matokeo ya kushinda na kushindwa,” alisema Dogo Janja.

Aliongeza, “Diamond bado ni mshindi, alikuwa mtanzania pekee, kwa hiyo huu sio wakati wakumbeza, tumtie moyo ili aendelee kupambana zaidi,”

Diamond ni msanii pekee wa Tanzania ambaye alikuwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hiyo ambayo ilichukuliwa na msanii kutoka Afrika Kusini.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!