Thursday, June 30, 2016

Eti Rubi kwanini unamsongo wa mawazo?


Video mpya ya Yamoto Band imeachiwa mitaani mapema wiki hii bila ya mwanadada Ruby kuonekana japo ilitafutwa kiki kuwa Rubby anatoka kimapenzi na Dogo Aslay.

Baada ya Video mpya ya Yamoto Band kuingia mtaani mapema wiki hii bila ya mwanadada Rubby kuonekana japo ilitafutwa kiki kuwa Ruby anatoka kimapenzi na Dogo Aslay na hakuna kitu baada ya bendi kumwaga mchele kwenye 5 Selekt ya EATV na kusema kuwa Ruby kazidiwa.

Tukaona siyo mbaya kumtembelea Mkubwa Fella TMK na kumkuta anawanoa vijana wengine wapya wa muziki wa Taarab ambao yeye ameamua kuwaita Moyo Fleva TAR na tulipomuuliza kuhusu kutokuonekana kwa Ruby kwenye video ya Suu alikua na haya ya kuongea.

Mkubwa Fella alisema sababu ya Ruby kutotokea katika kideo hicho ni kutokana na msongo wa mawazo amabao ulipelekea kuchukua takribani wiki mbili wakiwa wanamsubiri lakini ilishindikana ndio wakaamua kuweka msanii nwingine kwa niaba yake.

Mkubwa Fella alilisitiza kuwa watu wamuelewe vizuri Ruby kwani yeye ni kama binadamu mwingine anapatwa na matatizo pia na wasichukulie kwamba anatatizo lolote na Yamoto Band licha ya kuwa na maneno maneno mengi juu ya kutoonekana kwake kwenye video hiyo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!