Sunday, June 19, 2016

Gigy Money Amteka Hussein Machozi


MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Hussein Machozi, ameweka wazi hisia zake za kumkubali Video Queen anayetikisa hivi sasa kwenye tasnia ya urembo, Gigy Money.
Hussein Machozi, ameliambia Swaggaz, kuwa ni warembo wachache mno wanaoweza kujiamini kama anavyojiamini, Gigy ambaye huweka mambo yake mengi wazi ili mashabiki wapate kumfahamu vyema.

Watu wengi wanamtafsiri vibaya, Gigy, mimi naona ni msichana anayejiamini, , anatambua thamani ya urembo wake ndiyo maana anafanikiwa tofauti na Video Queen wengi wanaopotea haraka kwa sababu hawajui wautumie vipi urembo wao,” alisema Hussein Machozi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!