Wednesday, June 8, 2016

Jeshi la Polisi laombwa kuimarisha ulinzi kwenye misikiti wakati wa mfungo.


Sheikh wa mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta ameliomba Jeshi la polisi mkoani Kagera kuimarisha ulinzi kwenye maeneo ya misikiti ili wawawezeshe waumini wa madhehebu ya kiislamu kushiriki kikamilifu kwenye ibada wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Sheikh Kichwabuta ametoa ombi hilo alipozungumza na waandishi wa habari ofisi kwake leo,amesema hali ya sasa kwenye maeneo ya nyumba za ibada sio salama zaidi hasa nyakati za usiku pia ameliomba shirika la umeme (Tanesco) katika mkoa wa Kagera lipunguze vitendo vya kukata umeme mara kwa mara kwa kuwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani waumini wa madhehebu ya kiislamu hufanya ibada za usiku.
 
Aidha amewahimiza waumini wa madhehebu ya kiislamu kutumia mfungo huo kuimarisha mshikamano kwa hasa kupendana,kusaidiana na pia wawe na utulivu wakati wa mfungo wa mwezi huo.
 
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!