Monday, June 27, 2016

Kanye West aelezea kilichomsukuma kutoa video ya Famous yenye mastaa walio uchi


Kanye West haishiwi vituko. Wikiendi iliyoisha alitoa video ya wimbo wake Famous aliomshirikisha Rihanna ikiwaonesha mastaa kibao akiwemo yeye na mkewe Kim Kardashian, Taylor Swift, Chris Brown, Rihanna na wengine wakiwa wamelala kitandani watupuVideo hiyo imesababisha mjadala mkubwa na Taylor anadaiwa kuchukizwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa Kanye mastaa wengine kibao walimuambia kuwa ‘wangependa kuwepo kitandani’ alipowaonesha video hiyo.

Amedai kuwa ilichukua miezi mitatu kukamilisha video hiyo na kwamba wazo lake la msingi ni umaarufu wa mastaa hao kama wimbo ulivyo.

Wengine waliomo kwenye video hiyo ni pamoja na George W. Bush, Donald Trump, Anna Wintour, Ray J, Amber Rose, Caitlyn Jenner na Bill Cosby.

“Labda kwenye ulimwengu mwingine mimi na George Bush tungekuwa marafiki,” alisema. “I could have been his O.J. Simpson black friend on the golf course.”

Jumamosi West aliandika kwenye Twitter: Can somebody sue me already #I’llwait japo ameifuta tayari.Ni Chris Brown pekee aliyejibu tangu video hiyo itoke.

“Why I gotta have the plumbers butt/ crack showing WAX figure? This nigga KANYE CRAZY, talented, but crazy,”aliandika kwenye Instagram.

“Famous,” wimbo uliopo kwenye album yake The Life of Pablo album, ina mashairi makali kuhusu Taylor Swift: I feel like me and Taylor might still have sex / Why? / I made that bitch famous.”

Nasema mistari mingi wake wengine wasingewaruhusu waume zao waiseme,” West alisema kwenye mahojiano na Vanity Fair. “Lakini mke wangu pia hutoa picha ambazo waume wengine wasingewaruhusu waziweke. Moja ya funguo za kuwa na furaha kwenye ndoa yetu ni kwamba tunaruhusiwa kuwa wenyewe.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!