Monday, June 20, 2016

Vigogo Wazidi Kuchokoza Wizara ya Ardhi... wapora zaidi ya Hekari 2180 za Ardhi Morogoro

Migogoro ya Ardhi imeendelea kuwa gonjwa sugu kwa wananchi wasiojiweza licha ya serikali kuhaidi kuendelea kuitatua na kushughulikia.

Hali hii imetokea  jana ambapo, Wakazi wa kijiji cha Kilosa kata ya Mvuni iliyoko wilaya ya Morogoro., Mkoani Morogoro wakishirikiana na Viongozi wao wa kata, wamemuomba waziri wa ardhi, nyumba na makazi ,William Lukuvi, kuingilia kati mgogoro  wa ardhi kati yao na mwekezaji ambaye anadaiwa kufanya dhulma ya Hekari zaidi ya 2180 Wilayani humo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mvumi  ,Abdu Tumbo,  amesema kuwa ni mgogoro wa muda mrefu ambao umekuwa sugu katika kijiji hicho ambapo muwekezaji amekuwa akinyanyasa wananchi wenye haki ya maeneo yao
Tumbo ameeleza kuwa, Eneo la Muwekezaji huyo anayefahamika kwa jina la Pateli ni hekari 524 ambazo ameweka wafugaji lakini sasa amekuwa akizidi kuchukua mashamba ya watu wengine na kuweka wakulima na kukodisha mashamba ya watu waishio Wilayani humo.

Kwa upande wa Mfugaji Kidanyenye Kidasaki, amesema kuwa wanaomuomba Waziri Lukuvi aende eneo hilo ili  kutatua kero hiyo ya muda nmrefu kwani wafugaji katika eneo hilo wamekuwa wakinyanyaswa na kufukuzwa pia kuhamisha mara kwa mara mpaka mifugo yao inakufa bila hatia kwa sababu ya kuhama.

Aliongeza kuwa  kuwa kila mwezi muwekezaji Pateli anakuja kuchukua laki 4  kwa sababu ya wao kutumia eneo hilo ambalo sio lake.Kabushi Mateu ambaye ni Mkulima, amesema kuwa wakulima wamekuwa wakinyanyasika na hali ya uchumi ilivyokuwa ngumu kwani wamekuwa wakipangiwa fedha kubwa katika kukodi eneo la kulima, ambapo Naibu Katibu mkuu wa kikundi cha wakulima  kijiji cha Mvumi, Asha Kurususu ,amesema kuwa hali ya kiuchumi kwao inazidi kuwa mbaya kila uchwao ni vyema mamlaka husika zikalitatutua hilo kwa ustawi wa wananchi wake.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!