Saturday, June 18, 2016

Lollypop akanusha kuandika Ibaki Story ya Rich Mavoko


Producer, mwandishi wa nyimbo za Bongo Flava na muimbaji wa nyimbo za injili, Goodluck Gozbert ama kama anavyojulikana pia kama Lollypop, amekanusha kuandika wimbo wa Rich Mavoko, Ibaki Story.

Tetesi hizo zimekuwepo wiki hii na Rich tayari amezungumzia na kudai kuwa kuna vitu kadhaa Lollypop aliweka kwenye wimbo huo lakini si kwamba aliandika.
 
Akiongea nasi muimbaji huyo alisema: "Mavoko tunafahamiana na tumewahi kuonana mara chache lakini kuhusu hiki kinachoendelea kutrend kwakweli sifahamu na tumewasiliana pia kuhusu hili akaniambia anashangaa, nikamuambia mimi pia nashangaa kuhusu hilo kwahiyo ni kitu ambacho sielewi kimetokana na nini na ni kwanini kinazungumzwa.”“Ni tetesi tu na hazina ukweli wowote,” amesisitiza.

Msikilize hapo chini.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!