Friday, June 3, 2016

Mama Janeth Magufuli amshukuru TB Joshua kwa kuuunga mkono jitahada zake za kusaidia wazee.


Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli amewataka Watanzania kuiga mfano wa Mhubiri wa Nigeria, TB Joshua kwa kujitoa katika kuwasaidia wazee na watu wasiojiweza.

Mama Magufuli alisema hayo alipokuwa akitoa misaada katika Kituo cha Kaseka cha Wazee na Walemavu wa Ukoma kilichopo wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara.

“Niombe viongozi waliopo hapa kuhakikisha walengwa wanafaidika na misaada wanayopata, tayari nimepata malalamiko mengi kutoka kwa Wasukuma wenzangu kule Mwanza, yanavunja moyo.

‘‘Naomba  watu wasiuze wala kuiba hii misaada ni dhambi kubwa ukichukua chakula cha mtu mwenye mahitaji na asiyejiweza  hiyo ni laana itakufuatilia kwa sababu ni sadaka imeshaombewa,” alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!