Saturday, June 25, 2016

Mr Nice aachia albamu mpya ‘Kioo’, auza nakala 5000 nchini Kenya pekee

 
Msanii mkongwe wa muziki, Mr Nice Jumatano hii aliachia albamu yake mpya ‘Kioo’ ambapo mpaka sasa tayari ameshauza nakala 5000.
 
Akizungumza akiwa nchini Kenya, Mr Nice amesema albamu hiyo kwa sasa inapatikana nchini Kenya pekee.

“Kama nilivyohaidi kuwa sitembei na single kama wasanii wengine, natembea kiutuuzima zaidi kwa kutoa albumu,” alisema Mr Nice. “ahadi nimetimiza na mzigo umeingia sokoni rasmi na tayari nakala 5000 zimenunuliwa fasta ndani ya Kenya pekee,”

Aliongeza, “Nipo Kenya sasa katika tour kubwa kabisa ya kuitangaza albumu hii mpya na nina zaidi ya mwezi na nusu sasa ni show kwa kwenda mbele, after Kenya then ni Uganda halafu Rwanda na kwingineko kama ilivyo kawaida yangu, makoloni yangu yalipo napajua mimi mwenyewe.

 Nawashukuru sana mashabiki wa huko nyumbani Tanzania kwa kunisapoti na kuweza kunitia nguvu na hamasa kwa kipindi chote nilichokuwa nimetulia nikiandaa mambo na hatimae wakati umewadia na ahadi nimeitimiza sasa,”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!