Monday, June 6, 2016

Mufti Mkuu wa Tanzania Awataka Waislamu Waombee Amani ya Nchi

WAKATI Waislamu duniani kote wakitarajia kuanza kutekeleza moja ya nguzo tano za dini yao kwa kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Waislamu nchini kutumia mwezi huo, kuombe.

Aidha, wametakiwa kuhimizana kufanya kazi hasa katika kipindi hiki ili kupata riziki za halali kama kaulimbiu ya Rais John Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’ inavyosema kwa kaulimbiu hiyo si tu ni ya Rais, bali ni agizo la Mwenyezi Mungu kupitia kitabu chake Kitakatifu cha Kurani.

Hayo yameelezwa na Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Abubakar bin Zubeir wakati akizungumza kwenye Kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Mufti Zubeir alisema Rais Magufuli anaposema ‘Hapa Kazi Tu’ anakuwa amezungumzia dini moja kwa moja kwani hata katika Kitabu Kitukufu cha Kuran, Mwenyezi Mungu amesema anapendezwa na watu wanaofanya kazi.

“Kwa hiyo watu wahimizane kufanya kazi sana hasa katika kipindi hiki ili kupata riziki halali itakayowawezesha kupata mahitaji yao ya futari na daku,” alisema Mufti Zubeir. Aidha, aliwataka Waislamu kusaidiana ili kila mmoja afurahie mwezi wa Ramadhani.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!