Monday, June 20, 2016

Mwasiti adai anaogopa kuitoa kazi yake na Chidi Benz yasije yakamkuta ya Cyril na Raymond


Cyril aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa WCB baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Cheza kidogo’ akiwa amemshirikisha Raymond wa WCB, lakini baadaye uongozi wa WCB ulikanusha kwa kudai Raymond hakushirikishwa kwenye wimbo huo.

Mwasiti alisema kazi yake mpya na Chidi Benzi, aliifanya na rapper huyo kabla ya kuingia katika matitizo.

“Actualy kuna kazi tumeifanya na Chidi Benz, kali sana ila naogopa kuitoa yasije yakanikuta ya Kamikaze na Raymond, (huku akicheka) ila wakati ukifika nitaiachia, ni ngoma kali sana”, Mwasiti alikiambia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio.

Pia Mwasiti aliwahi kumshirikisha Chidi Benz kwenye wimbo wake uitwao ‘Hao’ ambao ulifanya vizuri.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!