Monday, June 13, 2016

Nchi za umoja wa Afrika zapongeza utendaji kazi wa Rais wa Tanzania.


Bodi  ya  ushauri  ya  kupambana  na  rushwa  na  ufisadi barani  Afrika (AUABC) imeelezea  kurishwa kwake  na hatua zinachukuliwa  na  serikali ya Tanzania kupambana na vitendo hivyo na imewataka viongozi  wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU)kuiga mfano wa Rais wa  Tanzania Mh Dr. John Magufuli wa kuonyesha kwa vitendo yale wanayozungumza kwenye majukwaa.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Bw Daniel Batidam amewaambia waandishi wa  habari jijini Arusha kuwa  kwa  sasa   asilimia kubwa  ya  wananchi   wa  nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU)wanamuona Rais wa Tanzania  Mh Dr John Pombe Magufuli kama mfano wa kuigwa kutokana na msimamo wake wa kuonyesha vitendo zaidi kuliko maneno katika kukabiliana na  rushwa,ufisadi na pia kusimamia uwajibikaji. 
kuhusu hali ya rushwa na ufisadi katika nchi za afrika Bw.Batidam  amesema pamoja na jitihada za taasisi mbalimbali za kupambana na  vitendo hivyo tatizo bado ni kubwa na linaendelea kuwaathiri wananchi wengi hasa wa kipato cha chini.
Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo kutoka nchi kumi na moja za Umoja  wa  Afrika waliokutana Arusha wamesema ili tatizo la rushwa na ufisadi liweze kupata ufumbuzi wa kudumu linahitaji ushirikiano mkubwa zaidi  hasa  kutoka  kwa   wananchi.
Katika kutambua mchango wa Tanzania katika masuala ya kukabiliana na  maovu mbalimbali nchi za umoja wa afrika zimeridhia makao  makuu  ya taasisi hiyo ya African Union Advisory Board  on Corruption  (AUABC)kujengwa Arusha Tanzania na mradi ambao unatarajiwa   kuanza  wakati wowote kuanzia  sasa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!