Tuesday, June 7, 2016

Nuhu Mziwanda katika penzi jipya

Baada ya kuachana na Shilole na kumwagana pia na aliyekuwa mchumba wake mwenye asili ya kiarabu Erah,Nuhu Mziwanda ameamua kupoza moyo wake kwa mpenzi mpya ambae amemchora tatoo.Akizungumza na Enewz Nuhu alisema kuwa anamshukuru mungu kwasababu mwanamke aliye nae ni mwanamke ambae amemuonyesha upendo kwa muda mfupi sana na anamuomba mungu kila siku amuweke kipenzi chake huyo na awe na moyo huo huo wa kumpenda zaidi.

Akizungumzia tatoo aliyochorwa na mwadada huyo Nawary, Nuhu alisema kuwa ni upendo wa hali ya juu ulioonyeshwa na msichana huyo baada ya yeye nae kumuonyesha upendo wake wa kweli na kudai kuwa hawajali watu wanazungumza nini juu yao ila yeye anampenda,anamuheshimu na hatoweza kumuangusha kamwe.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!