Thursday, June 16, 2016

Rais Dkt.Magufuli awataka wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula mwezi Mtukufu wa Ramadhan.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara nchini kutopandisha bei hususani zile za bidhaa za vyakula vinavyotumika kwa futari katika mwezi huu Mtukufu wa mfungo wa Ramadhani ili kuwapa wepesi waislamu kutekeleza moja ya nguzo muhimu za ibada yao bila shida.

Rais Dkt John Pombe Magufuli ameyasema hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwa utulivu na viongozi wa dini ya kiislamu pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo waliohudhuria mwaliko wake kwa kushiriki futari aliyowaandalia.
 
Aidha Rrais Dkt Magufuli waislamu kote nchini pamoja na watanzania kwa ujumla kuendelea kuliombea Taifa na kudumisha amani na mshikamano uliopo ili kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake.
 
Kisha Rais Dkt Magufuli akawatakia waislamu kote nchini mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwahakikishia kuwa kwa upande wa serikali itahakikisha uwepo wa usalama wa kutosha na amani.
 
Kwa upande wake Kaimu Mufti wa Tanzania Alhaji Hamid Jongo pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Musa Salimu wamesema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kupambana na ufisadi na kwamba watendelea kumuombea ili azma ya Rais ya kuliletea Taifa hili na maendeleo itimie.
 
Futari hiyo ilihudhuriwa pia na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na mke wa waziri mkuu Mary Majaliwa pamoja na viongozi na waamini wa dini ya kiislamu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!