Thursday, June 23, 2016

Rais Magufuli aeleza sababu kuu 2 za kusitisha ajira serikalini kwa muda


Katika hotuba yake kuadhimisha miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania, Rais John Pombe Magufuli amewatoa hofu wafanyakazi wa serikali kwa hatua ya kusitisha ajira serikalini kwa muda akielezea sababu kuu mbili za kuchukua uamuzi huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.

Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 Juni, 2016 katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, Mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!