Wednesday, June 15, 2016

Rais Magufuli amteua Mwenyekiti wa bodi TPA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Bw Ignas Aloyce Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa bodi ya ya Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania TPA kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia tarehe 21 April.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam hii leo Katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino (Idara ya uchukuzi) Dkt Leonard Chamuriho amesema kuwa Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Sheria na Mamlaka ya uteuzi huo Bw Rubaratuka ni Mhadhiri Mwandamizi katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Aidha kwa upande wake waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasilino Prof Makame Mbarawa amewateua wajumbea 8 wa bodi hiyo ikiwa ni pamoja na Eng Deuasdedith Kakoko, Bw Jaffeer Machano, Bw Malato Pachal, Dkt Jabir Bakari, Dkt Masanja Kadogosa, Bw Aziz Kilonje,Dkt Fransis Michael na Jyane Nyimbo ambao wote uteuzi wao umeanza tarehe 14 June.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!