Wednesday, June 29, 2016

Rais wa Zanzibar Awaapisha Watendaji wa Serikali hiyo


RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewaapisha viongozi mbalimbali kushika nyadhifa katika taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Walioapishwa ni Dk Islam Seif Salim kuwa Naibu Katibu Mkuu, Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Kabla ya wadhifa huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu iliyokuwa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Hassan Abdulla Mitawi ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Habari katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye kabla ya wadhifa huo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Zanzibar (ZBC).

Aidha, Dk Shein amemuapisha Rafii Haji Makame kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo. Alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) katika wizara hiyo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!